Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estominh Francis Chang'ah (wapili kushoto) akiwa na askari wa Jeshi la Polisi baada ya kukamata shehena ya viroba na madawa ya kulevya. |
Wilaya ya Ukerewe imepiga marufuku matumizi ya pombe
zijulikanazo kama viroba na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo bangi katika
kutekeleza adhma na agizo halali la Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya
Ukerewe Estominh F. Chang’ah ambaye ni mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa
Wilaya kwa kushirikiana na kikosi kazi kilichoundwa cha kupambana na matumizi
na biashara ya pombe aina ya Viroba, na madawa ya kulevya.
Shehena ya pombe aina ya viroba vilivyo kamatwa |
Kikosi kazi hiko kimefanya
msako na kimefanikiwa kukamata mfanyabiasha mmoja Pius Sanga aliyekutwa na katoni 128 za pombe aina ya
kiroba vyenye wastani wa gharama ya shilingi milioni 15.
Msako huo pia
umewezesha kukamatwa kwa mtu mmoja anaeitwa Kulwa Deo ambaye amekutwa na
misokoto 70 ya bangi na kilo moja (1) unga (madawa ya kulevya). Watuhumiwa wote
wanashikiliwa na jeshi la polisi na watafikishwa mahakamani.
“Watu kwa kiasi fulani
bado wanajihusisha na ulimaji wa bangi katika baadhi ya maeneo nawataka waache
mara moja kwani kikosi kazi bado kinaendelea na msako katika maeneo yote ya Wilaya
hadi visiwani”, alisema Chang’ah.
Shehena ya pombe aina ya viroba vilivyo kamatwa |
Kuendelea kutumia
viroba, bangi na dawa za kulevya ni hatari sana kwa afya ya binadamu kwani vina
athari mwilini, pia ni chanzo cha ajali kwani wapo waendeshaji wa vyombo vya
usafiri wa barabarani wanatumia hivyo ili kuepukana na matatizo hayo amewataka
watu kutokujihusiha kwani ni kinyume na agizo halali la Serikali.
Chang’ah amewataka
wananchi kuacha mara moja biashara ya viroba, bangi na dawa za kulevya kwani
yeyote atakae kamatwa na kikosi kazi kinachoendelea na msako atachukuliwa hatua
kali za kisheria. Ametoa rai kwa wananchi wema kushirikiana na jeshi la polisi
kwa kutoa taarifa kuhusu watu wanao jihusisha na bangi, dawa za kulevya na
viroba.
No comments:
Post a Comment