 |
Kutoka kushoto ni Kaimu Mweka Hazina(W) Baraka Munuo,katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Mhe. Frank Bahati kushoto kwake ni Afisa Utumishi Pelagia Sogoti na Afisa Ardhi na Maliasili Song'ora Nyango. |
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Frank Bahati amewataka watumishi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Ukerewe kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata sheria, kanuni na
taratibu za Utumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji wa kila mtumishi kwa
nafasi yake.
Bahati
ameyasema hayo alipofanya kikao na watumishi walioko ofisi za makao makuu ya
Ukerewe katika Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri, ambapo amesisitiza
kuwa watumishi wote kuanzia Wakuu wa Idara, Vitengo na watumishi wote kufanya
kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa na kuondokana na kufanya kazi kwa mazoea. Nanukuu
“wakati
wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha, kila mmoja kwa nafasi yake ahakikisha
anajituma kwa bidii na sio vinginevyo” alisema Bahati.
 |
Baadhi ya Watumishi wa Makao Makuu Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe |
 |
Baadhi ya Watumishi wa Makao Makuu Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe |
Bahati
amehimiza kuwepo kwa ushirikiano baina ya wafanya kazi kwani itasaidia kuleta
mahusiano mazuri na kuongeza ufanisi kazini. Ushirikiano ni jambo la muhimu na
watumishi wote wafanye kazi bila kuwa na matabaka. Kila Mkuu wa Idara ahakikishe
watumishi wote walio chini yake wana mahusiano mazuri ili kuweza kuwahudumia
wananchi wa Ukerewe kama inavyopaswa.
Ofisi
ya Mkurugenzi kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili kwa kushirikiana na Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya imeanzisha dawati la malalamiko ambalo wananchi wa Ukerewe
wanafika kwaajili ya kueleza malalamiko walionayo ili kuweza kupewa ufumbuzi wa
matatizo yao ya ardhi. Mpaka sasa ni malalamiko 35 yameshasikilizwa kupitia
dawati la malalamiko ya Ardhi na
walalamikaji kupewa majibu juu ya malalamiko yao. Dawati hilo linakaa kila siku
ya Jumanne katika Halmashauri ya Ukerewe Idara ya Ardhi na Maliasili. Bahati amewataka
Wakuu wote wa Idara wenye migogoro ya ardhi katika maeneo yao kuyaainisha na
kuleta taarifa juu ya migogoro hiyo kabla ya tarehe 30/10/2016 ili Idara ya
Ardhi iweze kushughulikia.
No comments:
Post a Comment