Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula(Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Ukerewe. |
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula(Mb) amefanya ziara ya kikazi Wilayani Ukerewe kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa Idara ya Ardhi Halmashauri na kuzungumza na watumishi. Ambapo alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estominh Chang’ah na kupokea taarifa ya Wilaya ambapo alielezwa kuwepo kwa changamoto ya ubovu wa injini ya kivuko cha abiria kinachobeba abiria kutoka eneo la Bugorola kuelekea kisiwa cha Ukara.
Katika hatua nyingine akipokea taarifa ya idara ya ardhi Naibu Waziri Angelina Mabula aliwataka idara iongeza nguvu katika shughuli zao za kila siku kwani hali ilivyo ya ukuaji wa mji na idadi ya watu inapanda kila siku, hivyo amewataka kuhakikisha upimaji wa ardhi unaendana na ukuaji wa mji na idadi ya watu ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Mabula amewataka watumishi wa idara hiyo kuwa waadilifu na kufanya kazi kama inavyopaswa na alisikitishwa kutokuwepo na matumizi ya Mfumo wa ukusanyaji malipo ya ardhi wakati mafunzo yalikwisha tolewa.
Mabula ameagiza Elia Mtakama ambaye anakaimu Ukuu wa Idara ya Ardhi na misitu kusimama mara moja nafasi yake ya Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya kwani hajaridhishwa na utendaji wake. “kuanzia sasa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Afisa Ardhi mteule Elia Mtakama hatakuwa tena mteule hivyo atafutwe afisa ardhi mwininge mwenye vigezo apewe kazi hiyo” alisema Mabula.
Mabula amesisitiza masijala ya ardhi iboreshwe na nyaraka zote zilizopo zinatakiwa zifanyie kazi kuwahudumia wananchi na kuwaondolea usumbufu.
No comments:
Post a Comment