Sunday, July 30, 2017

JAFO AIPONGEZA UKEREWE KWA UFANISI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akizungumza na watumishi kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estominh Chang'ah na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Frank S. Bahati na kulia kwakwe ni Mwenyekiti wa Halmashauri George Nyamaha na makamo Kalala Greygory.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) amefanya ziara Wilayani Ukerewe kwa dhumuni la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo ametembelea Hospitali ya Wilaya, vituo viwili vya afya ambavyo ni Nakatunguru na Muriti, mradi wa maji Lutare Chabilungo na miradi ya P4R ya mabweni, madarasa na vyoo katika shule za sekondari za Pius Msekwa na Bukongo na kishakuzungumza na watumishi wa halmashauri katika ukumbi mkubwa mikutano.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akikagua mitambo na akipokea maelezo kutoka kwa mkandarasi wa mradi wa maji Lutare Chabilungo
Naomba nishukuru sana Miradi mingi sana imefanya vizuri hongereni kwa kazi nzuri, nimetembelea mradi wa maji vijijini Lutare Chabilungo kazi imeenda vizuri na ninaamini tukisimamia mradi ule ipasavyo katika sehemu iliyobakia wilaya itakua na uwezo wa kupata maji vijijini kwa wastani wa 77% kutoka 55% hivyo usimamiwe vzuri mpaka mwisho. Alisema Jafo. Mradi unatekelezwa kwa bajeti ya Bilioni 7 ambapo mpaka sasa serikali imeshalipa Bilioni 5. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akimtwisha ndoo ya maji mama katika kijiji cha Lutare
Ametoa rai marekebisho yafanyike mapema na kama kuna mabomba yaliyo chini ya kiwango yasitumike ilikuiepushia Halmashauri gharama za kununua mabomba pindi mradi utakapo anza kazi. Amemuagiza injinia wa maji wilaya William Kahurananga kuhakikisha vijiji 13 vilivyo kwenye mradi vinapata maji.
Sekta ya afya imekua na changamoto ya upungufu wa dawa hivyo amemwagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Revocatus Cleophas kuhakikisha wananunua dawa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi “Pesa zote za kununua dawa zitumike kununua dawa na sio vinginevyo” alisema Jafo. Katika hatua nyingine amefurahishwa na matumizi ya mfumo wa malipo hospitali ukiwa unafanya kazi katika hospitali ya wilaya. 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akiwa ndani ya chumba cha upasuaji akipokea maelezo ya kutuo cha Afya Muriti
Akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri akizungumza nao amewataka watumishi wabadilike katika utendaji wa kazi maana “a business as usual” imekufa na amesema pamejengeka tabia ya watumishi kufanya kazi pekee zenye maslahi. Amewahimiza kuwepo na kipimo cha watumishi katika utendaji wa kazi na kuacha ubabaishaji. Hivyo tubadilike katika utendaji wetu wa kazi na tunaagana ni kwa uweledi gani tunatakiwa kufanya kazi.
Aidha Kupimana kazini kwa mfumo wa OPRAS system imekua haifanyiki ipasavyo katka maeneo mengi imekua ni ya (copy and paste) kama celebration form ya  harusi au zinafanyika pale wakaguzi au upandaji wa madaraja lakini katika sekta binafsi unafanya kazi na utendaji unapimwa hivyo watumishi wa serikali wanapaswa kubadilika na kuanza kuweka mpango kazi wa nini anatarajia kutekeleza lengo moja baada ya lingine na mkuu wa idara afanye hivyo na ikifika mwaka mwingine wa fedha uhakiki ufanyike kubaini malengo mliokubaliana yamefanyiwa kazi au la.
Wakuu wa idara wanaoshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo nafasi zao zijazwe na wengine kwani Halmashauri ina wataalamu wengi wazuri wenye elimu kuanzia shahada ya kwanza (Degree) na shahada ya uzamili (masters degree). “Lazima tubadilike”alisema Jafo.
Jafo alisisitiza kuwa tunapeana maelekezo ili tujirekebishe “ukitaka kuruka agana na nyonga”
Katika miradi ya elimu jafo alitembelea shule mbili za sekondari za pius msekwa na bukongo ambazo zililetewa fedha zaidi ya shilingi 500milioni kutekeleza ujenzi wa mabweni ya kulala wanafunzi mawili kwa kila shule, madarasa mannne kila shule na matundu ya vyoo.
Amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Frank S. Bahati kwani miradi mingi imetekelezwa katika ubora unaotakiwa na amewataka kurekebisha baadhi ya changamoto ilikuiletea ukerewe maendeleo  

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akikata mlango katika shule ya Sekondari Bukongo.No comments:

Post a Comment