Sunday, February 5, 2017

KIKAO KAZI CHA MAAFISA BIASHARA WA MKOA WA MWANZA CHA FANA.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Respicious Kagaruki (katikati) kulia kwakwe ni Anthony Y. Sikindene Afisa Biashara wa Mkoa wa Mwanza na Kushoto kwa Mkurugenzi ni Katwe Kisesa Afisa Biashara wa Ukerewe.


Wilaya ya Ukerewe imepata nafasi ya kupokea maafisa biashara wa Mkoa wa Mwanza ambao wamefanya kikao kazi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe. Akifungua kikao kazi hiko Kaimu Mkurugenzi wa Halmmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Respicious Kagaruki amewahimiza maafisa biashara kutumia kikao kazi hiko katika kujiimarisha katika utendaji wao na kutafuta suluhu ya changamoto wanazokabiliana nazo kwenye majukumu yao na kubwa hasa ni kujengeana uwezo na ufanisi mzuri baada ya kumaliza kikao kazi hiko.
 
Afisa Biashara wa Mkoa wa Mwanza Anthony Yesaya Sikindene akifafanua jambo katika kikao kazi cha maafisa biashara wa Mkoa wa Mwanza.



Afisa Biashara wa Mkoa wa Mwanza Anthony Yesaya Sikindene ametoa wito kwa Maafisa Biashara wa Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza kuendelea kutimiza majukumu yao vyema ili kuwaletea wana Mwanza maendeleo kwani Kitengo cha Biashara ni muhimu hivyo watambue kuwa wanajukumu kubwa kwa jamii.


Christopher Sinkala Mmoja ya watoa mada katika kikao kazi cha maafisa biashara wa mkoa wa Mwanza.


Mama Stella Rwakatare Mmoja ya watoa mada katika kikao kazi cha maafisa biashara wa mkoa wa Mwanza.

Maafisa Biashara wa mkoa wa Mwanza wamekutana Tarehe 4/2/2017 Wilayani ya Ukerewe kwa lengo la kujengeana uwezo hasa katika utendaji kazi wa kila siku ili kuweza kuongeza ufanisi.
Baadhi ya agenda zilizo wasilishwa na wawezeshaji ambao pia ni maafisa biashara ni pamoja na mada juu ya Leseni za biashara, leseni za Vileo, leseni za pikipiki na utumiaji wa mfumo wa kieletroniki n.k

Aidha Maafisa Biashara walitumia muda huo kumpongeza Afisa Biashara wa Mkoa wa Mwanza Mama Lucy Owenya ambaye amestaafu utumishi wa Umma na kumtakia kila lenye kheri katika maisha yake na kumpongeza kwa kazi nzuri na ushirikiano auliouonyesha kipindi akiwa mtumishi wa Serikali.

 
Maafisa Biashara wa Manispaa ya Ilemela.

Maafisa Biashara wa Manispaa ya Ilemela, Halmashauri ya Kwimba na Jiji.

Maafisa Biashara wa Halmashauri ya Ukerewe, Halmashauri ya Misungwi na Manispaa ya Ilemela.

Maafisa Biashara wa Mkoa wa Mwanza.

No comments:

Post a Comment