Friday, November 18, 2016

ZIARA YA MHE.SAMIA SULUHU HASSAN MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WILAYANI UKEREWE

Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomihn Francis Chang'ah akimpokea Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Ni ziara ya kwanza ya kihistoria kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika katika kisiwa cha Ukerewe. Akiwa katika Wilaya ya Ukerewe amefanya kazi kubwa mbili, ambapo ameweka mawe ya msingi katika miradi miwili ambayo ni Mradi mkubwa Maji Nansio na kituo cha upasuaji wa wakina mama Kagunguli.
Programu ya mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Ziwa Victoria (LVWATSAN-II) unatekelezwa katika miji kumi na tanoMradi huu ni moja ya miradi inayo wakilisha Umoja wa (15) iliyoko kwenye nchi tano (5) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Hati ya Makubaliano kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisainiwa. Kwa nchi ya Tanzania mradi huu unatekelezwa katika miji ya Sengerema, Geita na Nansio-Ukerewe.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ukerewe George Nyamaha akisalimiana na Mhe. Samia Suluhu Hassan alipo wasili Ukerewe
 
Mradi wa maji Nansio unategemewa kunufanisha watu 108,653, hali kabla ya mradi hapo awali ilikua hairidhishi hivyo kupelekea magonjwa ya milipuko hivyo kuwepo kwa mradi huu na mradi wa maji taka utasaidia kupunguza maradhi kama hayo.

Mradi wa maji Nansio umejengwa na Mkandarasi Angelique JV VISHWA kutoka India alisaini mkataba wenye thamani ya Tzs bilioni10.9 na maji taka mkandarasi MBESSO Construction Co. Ltd wa Dar es Salaam alisaini mkataba wenye thamani ya Tzs bilioni 2.259.





Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Frank Bahati akisalimiana na Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Eng. Gerson Lwenge (MB) ameitaka Wilaya na Halmashauri kutunza mradi huo kwa matumizi ya miaka mingi baadae na MWAUWASA ihakikishe wateja zaidi wanaunganishwa ili wanufaike na mradi. Aliishukuru Benki ya Afrika na kumalizia kwa kusisitiza kauli ya “Maji ni Uhai na Usafi wa Mazingira ni Utu”.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiweka Jiwe la Msingi katika mradi wa Maji Nansio.
Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji Nansio na kupongeza kwa hatua nzuri kuwa watu wengi wanatarajia kunufaika na huduma ya maji safi na salama, amewataka MWAUWASA ifanye kazi kwa karibu na Halmashauri hasa katika kutunza mitambo na wafanyakazi waajiriwe na wapate mafunzo ya kitaalamu kwani mradi ni mkubwa. Pia watu wakipata maji wataacha kuharibu mazingira hasa pembezoni mwa ziwa, hivyo amewaasa watu wa Ukerewe kuupenda mradi na kuutunza na pia kujenga makazi bora yenye vyoo vizuri kwani mradi wa majitaka upo hivyo taka zisipelekwe ziwani bali katika eneo lilipotengwa kwa ajili ya taka.
Makamu wa Rais baada ya Kuweka Jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Kagunguli.

Mhe. Samia Suluhu Hassan amepongeza Halmashauri kwa kutumia Mifumo wa kielektroniki katika kukusanya mapato hivyo amewahimiza watu kulipa ushuru na Halmashauri ikazane kukusanya mapato ya ndani, pia amepongeza mpango wa kupanda miti wa Wilaya ambapo Wilaya inatarajia kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka. Amesema haya akiwa kwenye viwanja vya michezo Kagunguli alipo ongea na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Kituo cha Afya Kagunguli cha Upasuaji kilichojengwa kwa ushirikiano na AMREF.
Mhe.Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi katika viwanja vya Kagunguli.
Ametoa pole kwa wahanga wa upepo mkali ulio athiri makazi ya watu na mali zao tarehe 4/11/2016  katika kata za Igalla, Mukituntu na Bwiro na kutoa msaada wa Mifuko 100 ya simenti na mabati 100. Makamu wa Rais amemaliza ziara yake Wilayani Ukerewe na kuahidi kurudi tena wakati mwingine.

No comments:

Post a Comment