Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe. John Mongella amefanya ziara ya Siku tano (5) Wilayani Ukerewe kwa dhumuni
la kukagua shughuli za Halmashauri na
miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa. Ili kuhakikisha sekta ya
elimu inakua na mabadiliko ambayo yataleta ufaulu na mazingira mazuri ya
wanafunzi kujifunza. Katika kuhakikisha hayo Mongella amefanya kikao na wadau
wa elimu Wilayani Ukerewe ambapo amewaweka pamoja walimu wa kuu na wakuu wa
shule zote, wenyeviti wa bodi za shule, maafisa elimu kata, maafisa tarafa,
watendaji, wadau wa taasisi zisizo za kiserikali na wataalamu wa elimu ngazi ya
mkoa katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri.
Mongella amewaasa
walimu kuwa na nidhamu ya kazi na uadilifu kwani wao ndio chanzo cha kuwa na
maendeleo kielimu pia wawe mfano wa kuigwa. “bodi za shule ziwajibike na
zisaidiane na uongozi wa shule kudhibiti nidhamu za watoto mashuleni” alisema
Mongella. Amepiga marufuku kuunda tume kwa mwalimu atakae mpa mimba mwanafunzi
na kesi za aina hiyo zisiwe za muda mrefu.
Amaewataka kuwepo na
usimamizi madhubuti wa fedha za elimu bila malipo kwa shule zote za msingi na
sekondari na fedha za serikali hizo zitumike kwa kufuata sheria, kanuni,
taratibu na miongozo na kuahidi kuleta timu yakukagua fedha hizo na namna
zilivyotumika na zinavyotumika na amewataka kurudisha hela kama mtu amezitumia
vinginevyo. Lengo kuu ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora kutokana na fedha
za elimu bure na historia inaonyesha ukerewe inauwezo mkubwa wa kufanya vizuri.
Wadau wa Elimu Wilayani Ukerewe |
Mongella amezitaka
kamati za shule na vikao vya wazazi vifanyike kila robo na visiishie
kuchangishana bali wazazi wa elimishwe katika maeneo ya kitaaluma na wote
wawajibike na taarifa na ratiba zipelekwe kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
John Mongella ametoa agizo juu wa ujenzi wa vyoo mashuleni ambapo amesema
kufikia mwezi agosti 30 pasiwe na shule yenye upungufu wa matundu ya vyoo, na
matundu ya vyoo katika shule yaende sawa na idadi ya wanafunzi na walimu katika
shule husika. “bodi ya shule na mkuu wa shule ambaye hatakua amejenga choo
itavunjwa” alisema Mongella. Pia amesisitiza bodi za shule na menejimenti za
shule zihusike katika ujenzi wa vyoo.
Pia alisikiliza
changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kupeleka mbale elimu wilayani
ukerewe na moja ya changamoto ni migogoro ya ardhi mashuleni hivyo akatoa
maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanaanza mara moja
upimaji wa ardhi katika shule ili kuepusha migogoro hiyo.
Mongella amewataka
maafisa elimu kata wawajibike katika kufuatilia shule zilizopo katika kata yake
na kuacha uzembe wa kutokutembelea shule. Wametakiwa kusisimamia mfumo wa elimu
kwenye kata na watoto wote wanatakiwa kwenda shule waripoti mashuleni, na
ametoa rai kazi kubwa ifanyike yakizalendo na hakuna kitakachotushinda.
Amesisitiza elimu ni sekta nyeti tusaidiane tuisukume ili twende mbele na
kufikia mafanikio.
Wadau wa Elimu Wilayani Ukerewe |
No comments:
Post a Comment