Wambura L. Kizito Mratibu wa Ustawi (M) akitoa mada wakati wa kikao kazi |
Mtoto
ana haki ya kulindwa na kutetewa pale anapotendewa ukatili ni wito uliotolewa
na Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza Wambura L. Kizito katika kikao kazi cha
Ulinzi na usalama wa mtoto ambacho kimefanyika katika ukumbi wa hospitali ya
Wilaya ya Ukerewe na kimewaweka meza moja wadau kutoka makundi mbalimbali wenye
wajibu wa kumlinda mtoto kama maafisa ustawi, mwendesha mashitaka, hakimu
mfawidhi, polisi, viongozi wa dini, NGO’s, wawakilishi wa watoto,idara ya maendeleo
ya jamii, idara ya elimu msingi na sekondari na idara ya afya.
Washiriki wakisikiliza mada |
Watoto
hukumbana na ukatili mbalimbali katika maeneo mbalimbali wanapokuwepo, baadhi
ya ukatili wanaokutana nao watoto ni pamoja na ukatili wa kihisia ambapo mtoto
anakutana na matusi, kinyimwa chakula, kuto thaminiwa, ukatili wa kimwili
inaambatana na vipigo,kukatwa viungo vya mwili, kuchomwa moto, kutumikishwa,
ukatili wa kingono inahusisha kubakwa, kulawitiwa, kuguswa maeneo binafsi,
kunajisi na ndoa za utotoni.
Wambura L. Kizito Mratibu wa Ustawi (M) akitoa mada wakati wa kikao kazi |
Lengo
la uwezeshaji ni kuhakikisha mtoto analindwa na Halmashauri inanafasi ya kuweka
mifumo madhubuti ambayo itamtunza na kumthani mtoto na kufuata sera, kanuni na
taratibu mbalimbali za kumlinda mtoto na zitasaidia kukabiliana na mila na
desturi zisizo rafiki pamoja na rasilimali watu wenye mafunzo na uzoefu wa
kutosha katika kumlinda mtoto.
Dkt.Titus Kaniki akichangia mada wakati wa kikao kazi |
Kizito
ameeleza huduma mbalimbali wanazohitaji watoto wanapofanyiwa ukatili ni pamoja
na afya,matibabu, sharia, malezi, ushauri nasihi, elimu na ulinzi na amewataka
wajumbe kuwahamasisha jamii kuwa walinzi wa watoto kwani mtazamo wa kijamii
mtoto akifanyiwa ukatili mara nyingi anasemwa vibaya na wengine wanatengwa.
Wambura L. Kizito Mratibu wa Ustawi (M) akitoa mada wakati wa kikao kazi |
Katika
utekelezaji Mahakama na jeshi la polisi
wanapaswa kujengewa uwezo wa namna bora za kumhudumia mtoto kwani kuna hitaji
kuangalia umri na jinsi yake. Hivyo wajumbe wote waliohudhuria mafunzo hayo
wametengeneza timu ambayo itahakikisha usimamiaji wa ulizi na usalama wa mtoto,
utoaji wa taarifa, elimu na uhamasishaji wa kumlinda na kumthamini mtoto dhidi
ya ukatili.
No comments:
Post a Comment