|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ukerewe Mhe. George Nyamaha akiteketeza zana za uvuvi haramu |
Idara ya Uvuvi na Mifugo imeendesha zoezi
lakukamata zana haramu za uvuvi ambapo imefanikiwa kukamata vitu hivyo ambavyo
vimekuwa vikitumiwa katika uvuvi ambao umekua ukiharibu mazalia ya samaki na
kupelekea kupungua kwa viumbe hao ziwani.
|
Moses Nduligu Mkuu wa idara ya Uvuvi na mifugo akifafanua jambo |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
ametoa rai kwa wananchi wa Ukerewe ambao shughuli yao kuu yakujipatia kipato ni
Uvuvi hivyo amewasihi kuachana na uvuvi haramu kwani ni mbaya na endapo
watakamatwa watachukuliwa sheria kwa vitendo hivo. Ameyasema hayo alipokua
akiongoza zoezi la uteketezaji wa zana hizo haramu kwa mazalia ya samaki na
viumbe vyake.
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ukerewe Mhe. George Nyamaha akiteketeza zana za uvuvi haramu |
Zana zilizokamatwa na kuteketezwa katika shimo la
taka la wilaya Bukongo ni makokoro ya sangara (bs) 5, makokoro vyambo/dagaa
(ss) 13, nyavu za timba 173, nyavu za makila macho chini inchi6 zipo 15,kamba
za kuvutia kokoro mita 2300. Zana hizi kwa ujumla zina thamani ya Tsh 75,040,000 .
|
Zana haramu zikiteketea Ukerewe. |
No comments:
Post a Comment