|
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akizungumza na watumishi kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estominh Chang'ah na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Frank S. Bahati na kulia kwakwe ni Mwenyekiti wa Halmashauri George Nyamaha na makamo Kalala Greygory. |
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani
Jafo (Mb) amefanya ziara Wilayani Ukerewe kwa dhumuni la kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo ambapo ametembelea Hospitali ya Wilaya, vituo viwili
vya afya ambavyo ni Nakatunguru na Muriti, mradi wa maji Lutare Chabilungo na
miradi ya P4R ya mabweni, madarasa na vyoo katika shule za sekondari za Pius
Msekwa na Bukongo na kishakuzungumza na watumishi wa halmashauri katika ukumbi
mkubwa mikutano.
|
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akikagua mitambo na akipokea maelezo kutoka kwa mkandarasi wa mradi wa maji Lutare Chabilungo |
Naomba
nishukuru sana Miradi mingi sana imefanya vizuri hongereni kwa kazi nzuri,
nimetembelea mradi wa maji vijijini Lutare Chabilungo kazi imeenda vizuri na
ninaamini tukisimamia mradi ule ipasavyo katika sehemu iliyobakia wilaya itakua
na uwezo wa kupata maji vijijini kwa wastani wa 77% kutoka 55% hivyo usimamiwe
vzuri mpaka mwisho. Alisema Jafo. Mradi unatekelezwa kwa bajeti ya Bilioni 7
ambapo mpaka sasa serikali imeshalipa Bilioni 5.
|
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akimtwisha ndoo ya maji mama katika kijiji cha Lutare |
Ametoa
rai marekebisho yafanyike mapema na kama kuna mabomba yaliyo chini ya kiwango
yasitumike ilikuiepushia Halmashauri gharama za kununua mabomba pindi mradi
utakapo anza kazi. Amemuagiza injinia wa maji wilaya William Kahurananga kuhakikisha
vijiji 13 vilivyo kwenye mradi vinapata maji.
Sekta
ya afya imekua na changamoto ya upungufu wa dawa hivyo amemwagiza Kaimu Mganga
Mkuu wa Wilaya Dr. Revocatus Cleophas kuhakikisha wananunua dawa kwa ajili ya
kuwahudumia wananchi “Pesa zote za kununua dawa zitumike kununua dawa na sio vinginevyo”
alisema Jafo. Katika hatua nyingine amefurahishwa na matumizi ya mfumo wa
malipo hospitali ukiwa unafanya kazi katika hospitali ya wilaya.
|
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akiwa ndani ya chumba cha upasuaji akipokea maelezo ya kutuo cha Afya Muriti |
Akiwa
katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri akizungumza nao amewataka watumishi
wabadilike katika utendaji wa kazi maana “a business as usual” imekufa na amesema
pamejengeka tabia ya watumishi kufanya kazi pekee zenye maslahi. Amewahimiza
kuwepo na kipimo cha watumishi katika utendaji wa kazi na kuacha ubabaishaji.
Hivyo tubadilike katika utendaji wetu wa kazi na tunaagana ni kwa uweledi gani
tunatakiwa kufanya kazi.
Aidha
Kupimana kazini kwa mfumo wa OPRAS system imekua haifanyiki ipasavyo katka
maeneo mengi imekua ni ya (copy and paste) kama celebration form ya harusi au zinafanyika pale wakaguzi au upandaji
wa madaraja lakini katika sekta binafsi unafanya kazi na utendaji unapimwa
hivyo watumishi wa serikali wanapaswa kubadilika na kuanza kuweka mpango kazi
wa nini anatarajia kutekeleza lengo moja baada ya lingine na mkuu wa idara
afanye hivyo na ikifika mwaka mwingine wa fedha uhakiki ufanyike kubaini
malengo mliokubaliana yamefanyiwa kazi au la.
Wakuu
wa idara wanaoshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo nafasi zao zijazwe na
wengine kwani Halmashauri ina wataalamu wengi wazuri wenye elimu kuanzia shahada
ya kwanza (Degree) na shahada ya uzamili (masters degree). “Lazima tubadilike”alisema
Jafo.
Jafo
alisisitiza kuwa tunapeana maelekezo ili tujirekebishe “ukitaka kuruka agana na
nyonga”
Katika
miradi ya elimu jafo alitembelea shule mbili za sekondari za pius msekwa na
bukongo ambazo zililetewa fedha zaidi ya shilingi 500milioni kutekeleza ujenzi
wa mabweni ya kulala wanafunzi mawili kwa kila shule, madarasa mannne kila
shule na matundu ya vyoo.
Amempongeza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Frank S. Bahati kwani miradi
mingi imetekelezwa katika ubora unaotakiwa na amewataka kurekebisha baadhi ya
changamoto ilikuiletea ukerewe maendeleo
|
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akikata mlango katika shule ya Sekondari Bukongo. |