Wednesday, March 8, 2017

Wanawake Ukerewe wahamasishana kuwa chachu ya maendeleo kiuchumi





Kauli Mbiu, “Tanzania ya viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi”

Wanawake Wilayani Ukerewe wamehamasishwa kuwa chachu ya maendeleo ya Uchumi wa viwanda kwani wana nafasi sawa kama wanaume hivyo wanatakiwa kujishughulisha kwa kuanzisha umoja ambapo wataweza kupata mikopo na kuweza kufanya mabadiliko kwa kuanzisha miradi yenye tija kwa familia zao na taifa kwa ujumla. Ameayasema hayo Winnifrida Gerati katinu wa UWT-Ukerewe katika maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika wilayani Ukerewe.

Wanawake wilaya Ukerewe wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kufanya maandamano kuanzia ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe na kuelekea Hospitali ya Wilaya na Magereza.
Wanawake hao wakiongozwa na katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (W) na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ukerewe pamoja Asasi mbalimbali zisizo za kiserikali wamewezesha na kufanikisha adhma ya kwenda katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe ambapo waliweza kugawa zawadi muhimu kwa matumizi ya wagonjwa wawapo wodini Kama vile sabuni na mafuta ya kujipaka.
Nae Matroni wa Hospitali mama Rutagarama amewapongeza kwa kuadhimisha siku hiyo kubwa ya wanawake duniani kwa kwenda kuwaona wagonjwa na kuwatia moyo. Nae Daktari Sundi Kamuli amewapongeza wanawake wenzake kwa kuonyesha moyo wa upendo kwa wenzao na kuwasihi matendo hayo yasishie siku za sherehe hizi tu bali hata siku za kawaida.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya ukerewe Song’ora Nyango aliwasindikiza wanawake katika kuadhimisha siku hiyo kwa kuwajulia hali wagonjwa walio lazwa katika wodi mbali mbali kama vile wodi ya wazazi, wodi ya wanawake na wodi ya Mama Ngojea. Rosemary Masunu ni mmoja wa wagonjwa walio pata zawadi za wanawake na amefurahishwa kwa moyo wa upendo na ushikamano ulioonyeshwa na wanawake wenzake na amewasihi kuendelea kua na moyo huo huo.
Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wanawake pia wamewatembelea wafungwa walipo gereza la wilaya na kuwatia moyo kwa kuwapa zawadi mbalimbali kwa matumizi yao ya kila siku, nao kwa furaha hawakusita kuwapongeza wanawake kwa moyo wa ushujaa na kuwatambua kuwa wao pia bado ni sehemu ya jamii ijapokua gereza hilo halina wanawake lakini wamewatembelea. Sp. Oswald Johson Bankobeza amepokea zawadi hizo na kuwashukuru kwa moyo wakipekee walionao wanawake wa Ukerewe.
Katika kufanikisha siku hiyo kubwa muhimu wanawake wamesindikizwa Asasi mbalimbali kama ULAO, HUNAU CBO, LVC na PO. EMEDO wamehimizwa kujihusisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi na ujasiriamali kwani wao ndio chachu ya maendeleo katika jamii Wamehamasishwa kujiendeleza kielimu kwani ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii.
  

Wanawake wakiwa katika maandamano katika siku ya wanawake duniani
wadau wakiwa na mabango yenye jumbe mbali mbali kuhusu mwanamke

Mmoja wa wadau waliojitokeza kuwasindikiza wanawake katika sikukuu yao
Mmoja ya wanawake akimkabidhi zawadi mama mzazi



Mkuu wa Magereza Ukerewe pamoja na maaskari magereza wakiwa pamoja na wanawake baada ya kupokea zawadi

No comments:

Post a Comment